Posts

MKASA WA KWELI NDANI YA NDOA 2

Image
Baada ya dakika 45 PETER aliingia akiwa anahema kwa wasiwasi uliompata kutokana na yale ambayo niliyomueleza kuwa yametokea nyumbani kwake.Alimpita house girl ambaye alikuwa akiendelea kumbembeleza mtoto barazani na kuja moja kwa moja mpaka sitting room na kukaa karibu na mkewe huku akimuinua kichwa.JESCA ambaye baada ya kumuona mumewe ameingia na kumuinua kichwa huku akimuuliza kulikoni, alimsukuma mumewe na kutoa sauti kali iliambatana na maneno ambayo yalizidi kumchanganya PETER. "Niacheeee!unaniinua kichwa ili nikuambie nini!hivi makenika anaweza kuijua gari kuliko alieitengeneza kiwandani?Hivi mimi nitakuwa na la kuambia kuliko wewe ulietenda!unataka kusema hauzijuhi!au haukuziweka wewe!Umesahau kuwa umenioa nikiwa na degree yangu!unalipi la kuniambia!nini bahati mbaya!au ndio uovu wako unataka kumsingizia shetani!haya niambie kuwa shetani alikupitia!ili nikuulize kilichopelekea upange ahadi ya kukutana mpaka amekupitia!". JESCA alitokwa na maneno mfululizo bila hata y

MKASA WA KWELI NDANI YA NDOA 1

Image
Ufuatao ni mkasa ambao umemtokea Jesca.Jesca ni binti wa miaka 24 ambae ameolewa na Peter.Ni Miaka miwili sasa toka walipofunga ndoa,katika muda wote wa maisha yao ya uchumba mpaka walipofunga ndoa waliishi kwa upendo,Amani,mafanikio na Amani kubwa sana katika maisha yao. Tabia zao ambazo walikuwa nazo kabla ya uchumba na hata baada ya uchumba ziliwafanya wao,wazazi wao na hata wanafunzi wenzao katika chuo walichokuwa wanasoma kuamini na kuwatabiria kuwa kila mmoja kati yao amepata mtu sahihi.Mahusiano hayo yaliwapeleka katika uchumba ambao uliwafanya situ mke na mume lakini pia uliwapa zawadi ya furaha kwao nayo ni motto pekee wa kiume Herman, Kutokana na mtoto huyo maisha yao yaliendelea kunawari kwa maelewano na uaminifu mkubwa na hapakuwa na mabadiliko yoyote ambayo labda yangeleta dosari au msukosuko katika ndoa yao yenye muda wa miaka miwili na motto mmoja. Hivi ni nani ambae asingependa maisha ambayo Jesca na Peter waliishi? Maisha ya ndoa yanamisukosuko mingi lakini kub