MKASA WA KWELI NDANI YA NDOA 1


Ufuatao ni mkasa ambao umemtokea Jesca.Jesca ni binti wa miaka 24 ambae ameolewa na Peter.Ni Miaka miwili sasa toka walipofunga ndoa,katika muda wote wa maisha yao ya uchumba mpaka walipofunga ndoa waliishi kwa upendo,Amani,mafanikio na Amani kubwa sana katika maisha yao.
Tabia zao ambazo walikuwa nazo kabla ya uchumba na hata baada ya uchumba ziliwafanya wao,wazazi wao na hata wanafunzi wenzao katika chuo walichokuwa wanasoma kuamini na kuwatabiria kuwa kila mmoja kati yao amepata mtu sahihi.Mahusiano hayo yaliwapeleka katika uchumba ambao uliwafanya situ mke na mume lakini pia uliwapa zawadi ya furaha kwao nayo ni motto pekee wa kiume Herman,
Kutokana na mtoto huyo maisha yao yaliendelea kunawari kwa maelewano na uaminifu mkubwa na hapakuwa na mabadiliko yoyote ambayo labda yangeleta dosari au msukosuko katika ndoa yao yenye muda wa miaka miwili na motto mmoja.
Hivi ni nani ambae asingependa maisha ambayo Jesca na Peter waliishi? Maisha ya ndoa yanamisukosuko mingi lakini kubwa ambalo hufanya ndoa nyingi zivunjike na ukosefu wa uaminifu na tamaa.Hili kwa kina JESCA na PETER halikuwepo hata kidogo.Simu zao hazikuwa na password na wala haijawhi kutikea mmoja wao kumkataza mwenzie kushika au kupokea simu ya mwenzake,lakini pia haikuwahi kutokea mmoja wao kupigiwa simu na asipokee mbele ya mwanzake,maisha yao yalijaa uaminifu wa hali ya juu na upendo usionakifani.
Maisha yao yaliwavutia wengi na hasa wale ambao waliokuwa na migogoro katika ndoa zao,walishindwa kujua siri ya mafanikio ya wanandoa hao!.Siku zilipita na mmaisha yakawa matamu kwa upande wao.Lakini leo nimepita nyumbani kwao kuwajulia hali.Ila nilichokikuta na kukisikia nilishindwa kukiamini lakini pia nimeshindwa kumshauri Jesca juu ya hili kutokana na hali niliomkutanayo.Jesca niliemkuta leo sio yule niliemjua!hakuwa na furaha kiasi cha kwamba nilijuta kwanini nilienda kuwajulia hali!.
Ukiachilia mbali mtoto ambae licha yakuwa amebebwa na kubembelezwa na house girl ambae pia alipoteza furaha kwa hali iliyokuwa hapo nyumbani.Kwa kweli hali nilioikuta ilinihuzunisha sana na nilijitahidi kuuliza nini kilichojiri mpaka kukawa na hali hiyo,jibu la swali langu hilo halikupatikana kwa urahisi kwani hata house girl ambae labda angeweza kuniambia pia alikuwa hajui sababu iliyopelekea boss wake kulia!.
Baada ya jitahada za kutaka kujua nini kilichopelekea shemeji yangu JESCA kulia hali ya kuwa yupo peke
Hatimaye alipunguza kilio chake na akaanza kunieleza kile kilichopelekea yeye kulia kwa hasira na kwikwi na haya ndiyo aliyonieleza;
“Shemeji Hamisi huwezi kuamini na wala sikudhani kama mme wangu ana tabia kama hizi!ama kweli kuwa uyaone na sasa nayaona!nilikuwa nikijamini kuwa ninathamani na ninapendwa na mme wangu toka kipindi tupo chuo lakini kumbe sikuwa na thamani kama ambavyo nilivyokuwa ninafikiria!Nimevuka nguo!natamani ardhi ipasuke ili niingie nikajifiche!kweli Mungu hamfichi mnafiki!sikufikiria wala sikudhani kama mme wangu anatabia hizi!naamini alikuwa akifanya siri na sasa ameamua anionyeshe dhahiri!PETER!PETER!PETER wakunifanyia mimi hivi!PETER wakufikia hatua ya kufanya hivi!leo naamini mapenzi hayana mdhamana!kweli amini kuwa unapenda ila usiamini kama unapendwa!hivi upendo na uaminifu wangu kwa mume wangu kweli nillistahili kuyakuta haya niliyoyakuta!”.
JESCA aliendelea kulalamika bila ya kuweka wazi kile anachomaanisha,niliamua kumpigia simu rafiki yangu PETER ili anijuze kafanya nini mpaka hali imekuwa hivi,lakini alishangaa na kutoamini kile ninachokiona na kukisikia nyumbani kwake!baada ya kumthibitishia uhalisia wa kile ninachokiona alianihakikishia kuwa anatoka ofisini muda si mrefu atakuwa amefika nyumbani.

                                                                                                                                                                                              
“Shemeji HAMISI naumia sana,sikustahili hiki!hivi PETER wakuniwekea condom kwenye suruali yake!nimekuta condom hii ambayo haifunguliwa na pakiti hii ya condom ambayo imetumika!”.
JESCA alinionyesha condom ambayo alidai ameikuta kwenye mfuko wa suruali ya mumewe pindi alipokuwa anafua na pia alinionyesha pakiti ya condom ambayo inaashiria kuwa condom yake ilitumika,
Hapa nilipo JESCA ameanza kulia tena kwa uchungu house girl na anajitahidi kumbembeleza motto ambaye kila akimuangalia mama yake anayetokwa na machozi nae anazidisha kilio na mama yake hawezi kumshika wala kumbembeleza motto!sijuhi PETER atakuja kusema nini!wakati namsubiri nimeona nikushirikishe ili unisaidie mawazo juu ya mkasa huu.Unaweza uvaa uhalisia wangu,JESCA au PETER Toa maoni yako wakati tunamsubiri PETER atueleze kulikoni.


Comments

MWALIMU

MKASA WA KWELI NDANI YA NDOA 2