MKASA WA KWELI NDANI YA NDOA 2

Baada ya dakika 45 PETER aliingia akiwa anahema kwa wasiwasi uliompata kutokana na yale ambayo niliyomueleza kuwa yametokea nyumbani kwake.Alimpita house girl ambaye alikuwa akiendelea kumbembeleza mtoto barazani na kuja moja kwa moja mpaka sitting room na kukaa karibu na mkewe huku akimuinua kichwa.JESCA ambaye baada ya kumuona mumewe ameingia na kumuinua kichwa huku akimuuliza kulikoni, alimsukuma mumewe na kutoa sauti kali iliambatana na maneno ambayo yalizidi kumchanganya PETER.
"Niacheeee!unaniinua kichwa ili nikuambie nini!hivi makenika anaweza kuijua gari kuliko alieitengeneza kiwandani?Hivi mimi nitakuwa na la kuambia kuliko wewe ulietenda!unataka kusema hauzijuhi!au haukuziweka wewe!Umesahau kuwa umenioa nikiwa na degree yangu!unalipi la kuniambia!nini bahati mbaya!au ndio uovu wako unataka kumsingizia shetani!haya niambie kuwa shetani alikupitia!ili nikuulize kilichopelekea upange ahadi ya kukutana mpaka amekupitia!".
JESCA alitokwa na maneno mfululizo bila hata ya kumpa mumewe nafasi ya kujua kinachomliza na kumpotezea amani.
"JESCA!".Aliita PETER.
"JESCA!una nini?mbona unasema maneno maneno ya shutuma na mafumbo ambayo mimi siyafahamu?umekutwa na nini mke wangu mpaka amani ya nyumba inapotea?ni kipi ambacho kinakufanya hata usijali kilio cha mda mrefu cha mtoto wetu mpendwa!ni kipi ambachokinakufanya hata mimi mumeo ushindwe kuniambia  unatoa mafumbo na maneno nisiyoyajua!".Alilalamika PETER.
JESCA bila kujibu aliinuka huku akilia kwa kwikwi na kwenda kujifungia chumbani.PETER alitaka kumfuata lakini nilimshika mkono kumzuia,kwani nilijua kuwa shauku yake kwanza ni kujua tatizo ninini,hivyo niliamini JESCA asingeweza kumwambia chochote kutokana na hasira alizo nazo ukizingatia alishasema"makenika hawezi kuijua gari kuliko alieitengeneza kiwandani"kwani JESCA aliamini mumewe anajua ila anajifanya hajuhi ili kujitetea.
PETER ebu kaa nikueleze,PETER alikaa kwenye sofa huku akiniangalia,unaona ile pale nilimuonyesha kwa kidole pakiti mbili za kondom,moja ambayo ilikuwa tupu na nyingine ilikuwa haijafunguliwa.
"Ndio nimeon"alijbu PETER.
Vizuri,mkeo anadai kuwa hizi kondom amezitoa kwenye mfuko wa nguo zako zikiwa hivyo yaani moja imetumika yaani pakiti isiyonakitu na nyingine ambayo bado ndani ina kondom yake.Nilipomueleza hivyo PETER alisimama huku akipiga piga paji lake la uso.
kondom kwenye nguo zake
 Alishusha pumzi nzito huku akiendelea kupiga paji lake la uso.
"Hili tu ndilo linalofanya amani ipotee!si angeniuliza!sasa atajuaje ukweli wa hili!mimi nilifanya hivi kwa maana yangu!nilitaka nijiridhishe!kwanini asiniulize ina maana haniamini!miaka yote tulikuwa pamoja tupo chuo,uchumba,ndoa mpaka tumepata mtoto nilishawahi kufanya hivi!aje aniulize nitamwambia".Alisema PETER kwa kujiamini.
Kama ni hivyo kaa acha mimi nimwite shemeji ili umueleze kulikoni.PETER alikaa na mimi niliinuka kwenda kumwita JESCA ambaye nahisi alikuwa anafuatilia mazungumzo ya PETER alipokuwa akiongea kwa sauti kwani kilio hakikusikika muda wote ambao PETER alipokuwa akizungumza.
Ndugu msomaji mimi namwita JESCA ili tumsikilize PETER anataka kusema nini kuhusiana na kondom kukutwa kwenye mfuko wa nguo yake.JE unahisi PETER atasema nini?Je hayo atakayosema PETER yatatatua tatizo?au yataongeza?Ebu changia maoni yako hapo chini wakati namwita JESCA.
Baada ya muda mchache nilifanikiwa kumshawishi Jesca kunyamaza na kufuatana na mimi mpaka alipokuwa Peter kwa ajili ya kusikilize kile ambacho Peter ameahidi kukisema kuhusiana na swala zima la kukutwa kondom kwenye nguo zake.
Mimi na Jesca tulikaa kwenye sofa na kumuachia uwanja Peter atiririke juu ya mkas mzima wa kukutwa na kondomu kwenye nguo zake na haya ndio yalikuwa maelezo yake.
"Ki ukweli sijawahi kumsaliti mke wangu toka kipindi tumeanza mahusiano kipindi kile tupo chou,kipindi cha uchumba wetu na hata kipindi cha ndoa yetu.Mke wengu anathamani kubwa sana kwangu na hili nalijua na kulithamini siku zote,hakuna ninachokosa kwa mke wangu,kama nimapenzi ananipa ya kutosha na kuniridhisha,kama mtoto amenizalia Zaidi ya hapo ananifanyia mambo mengi ya thamani ambayo sikutarajia lakini ananifanyia kwa namna anavyonipenda na kunithamini pia kunithibitishia kuwa yeye ni mke bora kwangu na hilo halina shaka kwani mimi ninajua kuwa yeye ni mke  bora kwangu.Swali la msingi ambalo najua mnajiuliza kama sijawahi kumsaliti mke wangu mbona kondomu zimekutwa kwenye nguo zangu?kabla sijaweka wazi kuhusiana na kondomu nataka nichukue dakika chache kueleza namna mke wangu ambavyo amekuwa akiniamini kiasi ambacho hajawahi hata siku moja kunihisi vibaya juu ya mahusiano yetu kabla ya ndoa na hata baada ya ndoa.Kwa kipindi chote mke wangu amekuwa akiniamini na kunithamini uaminifu ambao umepelekea mke wangu kutokuwa na shaka na mimi ni jambao zuri kwa hakika lakini bado lilikuwa likinipa shaka na wasi wasi kwa upande mwingine,Babu yangu alipokuwa ananifundisha maada ya kutimiza miaka kumi na nane aliniambia kuna siku nitakuja kuwa na mke na akaniambia mke bora kwangu ni yule anaenipenda kwa dhati na ambaye anaemia juu yangu na kupata tabu juu yangu ambae hapendi niende kwa mwingine na kumuacha yeye,mwanamke ambaye atakuwa ananichunga nisipotee kama ambavyo mchungaji anavyotazama mifugo yake isipotee.Dalili ya kujua mwanamke kama anakupenda ni witu!kwani mapenzi yanapozidi hayakosi wivu!hayo mafunzo ya babu niliyashika na kuamini kuwa kama kweli mke wangu ananipenda kama ninavyompenda atakuwa na wivu juu yangu!kwa hakika hata familia yake wanajua namna ninavyomuonea wivu mke wangu!hilo halina kiificho na hata yeye anajua!lakini hata siku moja mke wangu hajawahi kunionea wivu!Ninapochelewa au hata ninapoongea na simu hali ya kuwa mimi mengine niliyafanya ili mke wangu anionee wivu na niamini maneno niliyoambiwa na babu yangu kuwa mapenzi ya kweli hayakosi wivu!Nilifanya njia nyingi sana lakini hata siku moja mke wangu hajawhi kugundua kwamba nahitaji kuonewa wivu!ndipo usiku wa jana kuamkia leo nilinunua kondom tatu,moja nikaifungua na mbili nikaziacha bila kuzifungua,moja ambayo sijaifungua niliiweka kwenye mfuko wa shati pamoja na paketi iliyofunguliwa,na ile nyingine ambayo haijafunguliwa nimeiweka juu ya dirisha la bafuni pamoja condom iliyofunguliwa(mpira) na nilifanya hivi kama mtihani wa kumpima mke wangu kwani alinipa kila kitu ila alishindwa kunionea wivu tu kitu ambacho mimi nilikitam sana!.Kwa kuwa leo mke wangu umeumia kwa hili nimethibitisha kweli unanipenda na Zaidi ya hapo nimefurahi kuwa mke wangu kwa mara ya kwanza umenionea wivu!.Nakuthibitisha kuwa hizi kondomu zipo hapa ndani naomba tufuatane chooni nikawaonyesheni hizo kondomu zingine ambazo nilizihifadhi huko na zingine nikaziweka kwenye mfuko wa shati".
baada ya kusema maneno hayo Peter aliinuka huku akiituashiria tumfuate kuelekea chooni.mimi na Jesca pia tuliinuka na kumfuata na sikuamini kama Jesca pia angeinuka mwenyew bila ya kutumia nguvu kubwa ya ushawishi,huenda kuna kitu kilimvutia au kumfunza katika maelezo ya Peter.Tuliingia chooni wote watatu huku Peter akitangulia,akanyoosha mkono juu ya Dirisha na kuvuta kikaratasi kilichovingirishwa,alikifungua na kutuonyesha kile kilichokuwamo ndani ya karatasi hiyo,ni kweli mpira wa condom na pakiti nyingine ya kondomu ambayo ilikuwa haijafunguliwa.
Kwa furaha Jesca alikumbatia Mmewe huku machozi yakimtoka na Peter nae akamkumbatia mkewe kwa furaha na huku akimfuta machozi.
Hapa ndio mwisho wa mkasa huu wa kweli ambao umemuhusisha Peter na Mkewe Jesca.

Comments

  1. Casino Slot Machines Online - Dr.MCD
    With a wide 경산 출장안마 variety of casino 군포 출장마사지 slot 남원 출장안마 games, you can also play more slots on a mobile phone or tablet, whether you're from the 아산 출장안마 USA 영주 출장샵 or Canada.

    ReplyDelete

Post a Comment

MWALIMU

MKASA WA KWELI NDANI YA NDOA 1